1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Iran awasili Iraq katika ziara ya kwanza ya kigeni

11 Septemba 2024

Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian amewasili nchini Iraq leo, katika ziara yake ya kwanza ya kigeni tangu alipoingia madarakani.

https://p.dw.com/p/4kV3y
Masoud Pezeshkian na waziri mkuu wa Iraq Mohammed Shia al-Sudani(kushoto)
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian(kulia) akikagua gwaride mara baada ya kutua IraqPicha: Murtadha Al-Sudani/AP Photo/picture alliance

Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian amewasili nchini Iraq leo, katika ziara yake ya kwanza ya kigeni  tangu alipoingia madarakani.

Ofisi ya waziri mkuu wa Iraq, imefahamisha kwamba kiongozi huyo wa Iran alikaribishwa na waziri mkuu Mohammed Shia al Sudani, huku ikionesha picha za viongozi hao wakisalimiana katika uwanja wa ndege wa Baghadad. Kabla ya ziara hiyo kituo cha habari cha taifa nchini Iran kilisema Rais Pezeshkian, atasaini makubaliano kadhaa nchini Iraq ambako atakutana na maafisa wa ngazi za juu mjini Baghdad.

Pezeshkian ameahidi kutowa kipaumbele katika mahusiano na mataifa jirani wa Iran, kuiondowa nchi yake katika hali ya kutengwa kimataifa na kupunguza athari za kiuchumi nchini humo zinazotokana na vikwazo ilivyowekewa na nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani.

Iraq ambayo ni mshirika wa Marekani na Iran, ina wanajeshi 2,500 wa Marekani waliopiga kambi nchini humo, lakini pia ina wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran na wanaofungamanishwa na vikosi vyake vya usalama.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW