1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Iran awaonya wanaoishambulia Yemen

Sekione Kitojo
5 Desemba 2017

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Wayemeni watawafanya wale wanaoishambulia nchi yao wajutie vitendo vyao wakati  muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ukishambulia mji mkuu wa Yemen unaoshikiliwa na waasi.

https://p.dw.com/p/2om6v
Iran Rohani 100-Tage-Bilanz der Regierung
Picha: irna.ir

Mtoto wa rais wa  zamani  wa  Yemen Ali Abdallah  Saleh , aliyeuwawa na wanamgambo  wa  kihuthi , alitoa wito  wa  kulipiza  kisasi  dhidi  ya makundi  yanayoungwa  mkono  na  Iran.

"Watu  wa  Yemen  wanawafanya  wachokozi wajutie hatua walizochukua," Rouhani  amesema  katika  hotuba  iliyotangazwa moa  kwa  moja  katika  televisheni. Matamshi  yake  yanakuja  siku moja  baada  ya  kuuwawa  rais  wa  zamani  Ali  Abdallah Saleh na Wahuthi  wanaoungwa  mkono  na  Iran na  kusababisha mashambulizi  makali  kutoka  kwa  majeshi  yanayoungwa  mkon  na Saudi  Arabia  dhidi  ya  mji  mkuu  wa  Yemen Sanaa.

Jemen Ali Abdullah Saleh 2005
Rais wa zamani Ali Abdullah Saleh Picha: picture-alliance/dpa/Yahya Arhab

Kamanda  wa  vikosi  maalum  vya jeshi  la  Iran, Mohammad Ali Jafari , amesema  Saleh aliuwawa  kwasababu  alikuwa  akijaribu kuuondoa  uongozi  wa  Wahuthi  kutoka  madarakani.

Saleh  hivi  karibuni  alivunja  muungano  wake wa  mashaka uliodumu  kwa  muda  wa  mika  mitatu  na  Wahuthi  na  kusema yuko tayari kwa  mazungumzo  na  Saudia.

"Wasaliti  Saudi Arabia  wanataka  kuleta  hali  ya  wasi  wasi  wa kiusalama  katika  eneo hili chini  ya  amri  kutoka  Marekani wakifanyakazi  kwa  pamoja  na  Israel , tumeshuhudia juhudi  zao  za kuanzisha  mapinduzi  dhidi  ya  Wahuthi, ambayo yamekabwa mapema kabla  ya  kuzaliwa.

Jemen Ali Abdullah Saleh wurde ermordet
Wapiganaji wa Kihuthi mjini SanaaPicha: Reuters/K. Abdullah

Ndege  za  majeshi  ya  muungano  unaoongozwa  na  Saudi Arabia zimeshambulia  maeneo  ya  mji  mkuu  yanayoshikiliwa  na  waasi alfajiri ya  leo  baada  ya  waasi  kumuua  rais  wa  zamani  Ali Abdullah Saleh wakati  akikimbia  kutoka   mji  huo  kufuatia kuvunjika  kwa  muungano  wao , wakaazi  wa  mji  huo  wamesema.

Wito wa kupambana  na  Wahuthi

Rais  anayeishi  uhamishoni Abedrabbo Mansour Hadi  ametoa wito kwa  Wayemeni  kujiunga  pamoja  dhidi  ya  wapiganaji wanaoungwa  mkono  na  Iran. Karibu  mashambulio  saba yameangukia  katika  jengo  la makao  makuu  ya  rais  katika  eneo linaloishi  watui  wengi   katikati  ya  mji  wa  Sanaa, wamesema watu  walioshuhudia.

Kumekuwa  na mapambano  madogo  madogo  kati  ya  Wahuthi  na waungaji  mkono  wa  Saleh  katika  wilaya  za  kusini  ambazo zimekuwa  ni  ngome  kuu  ya  waungaji  wake  mkono.

Nae  mtoto  wa  rais  wa  zamani  Ali Abdullah Saleh  aliyeuwawa ametoa  wito  wa  kulipiza  kisasa dhidi  ya  makundi  yanayounga mkono  Iran.

Jemen Ali Abdullah Saleh wurde ermordet
Wanamgambo wa Kihuthi wakishangilia mtaani baada ya kuuwawa kwa Ali Abdullah SalehPicha: Reuters/K. Abdullah

"Nitaongoza  mapambano  hadi  Mhuthi  wa  mwisho atakapoondo9lewa  kutoka  Yemen, damu  ya  baba  yangu itasikika katika  masikio  ya  Iran, "  alinukuliwa  Ahmed Ali Saleh  akisema. Amewataka  waungaji  mkono wa  baba  yake , "kuirejesha  Yemen kutoka  mikono  ya  wanamgambo  wa  Kihuthi wanaoungwa  mkono na  Iran".

Mkuu wa Umoja  wa  nchi  ya  Kiarabu  Arab League  Ahmed  Abdul Gheit ameshutumu  leo  kuuwawa  kwa  rais  wa  zamani  wa  Yemen na  waasi  wa  Kihuthi, akisema  hali  hiyo  inaelezea  juu  ya  hali msingi  wa uhalifu wa  kundi  hilo. Mkuu  huyo  wa  jumuiya  ya mataifa  ya  Kiarabu  ameonya  kwamba  kuuwawa  kwa  Saleh  siku ya  Jumatatu  kunatishia  kuripuka kwa  hali  mbaya ya  usalama , katika  nchi  hiyo  iliyoharibiwa  kwa  vita.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre / afpe

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman