1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Rais wa Iran amteua katibu mpya wa baraza kuu la usalama

22 Mei 2023

Rais wa Iran Ebrahim Raisi amemteua jenerali Ali Akbar, kuwa katibu wa taasisi ya juu ya usalama na kumuondowa Ali Shamkani aliyekuwa akisimamia shughuli za usuluhisho katika eneo la Ghuba.

https://p.dw.com/p/4Rg1z
Ali Akbar Ahmadian - General Sekretär des iranischen Nationalsicherheitsrat
Picha: fararu

Kwa mujibu wa maelezo yaliyochapishwa katika tovuti rasmi ya rais, Ali Akbar Ahmadian anachukuwa uongozi wa baraza kuu la kitaifa la usalama  kwa amri ya rais ambayo pia imetengua uongozi wa takriban muongo mmoja wa Ali Shamkhani mwenye umri wa miaka 67 ambaye alibeba dhima muhimu katika makubaliano ya kihistoria ya kujongeleana tena kati ya Iran na Saudi Arabia mnamo mwezi March.

Ali Akbar aliwahi pia kuwa mwanachama wa baraza linalomshauri kiongozi wa juu kabisa nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei.