Rais wa Iran afanya ziara nchini Indonesia
23 Mei 2023Lengo la kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo yenye waumini wengi wa Kiislamu huku kukiwa na mivutano katika siasa za kimataifa.
Soma pia: Iran, Uturuki, Iran zatiliana saini mikataba ya kibiashara, kiuchumi
Widodo alimpokea kwa heshima zote za kiitifaki Ebrahim Raisikatika Ikulu ya Bogor iliyopo nje kidogo ya mji mkuu, Jakarta. Rais huyo wa Iran ameitembelea Indonesia kutokana na mualiko wa Widodo, kwani Indonesia ina lenga kufufua uchumi wake kwa kuongeza mauzo ya nje baada ya kuathiriwa na janga la Uviko-19.
Takwimu za mamlaka nchini Indonesia zimebaini kuwa biashara kati ya nchi hiyo na Iran katika kipindi cha Januari hadi Machi inakadiriwa kufikia Dola milioni 54.1, huku thamani ya biashara baina ya mataifa hayo ikiongezeka kwa zaidi ya asilimia 23 hadi kufikia dola milioni 257.2.