1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa IOC Thomas Bach aifunga rasmi michezo ya Olimpiki

12 Agosti 2024

Michezo ya Olimpiki ya Paris imefungwa rasmi na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, IOC, Thomas Bach hapo jana usiku.

https://p.dw.com/p/4jMZu
Rais wa IOC Thomas Bach
Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki - IOC Thomas Bach aliikabidhi Marekani bendera ya Olimpiki kwa ajili ya Michezo IjayoPicha: Jan Woitas/dpa/picture alliance

Bach aliifunga michezo hiyo iliyofanyika kwa mara ya tatu katika mji mkuu wa Ufaransa Paris, baada ya sherehe ya ufungaji ya kifahari iliyohusisha ukabidhi kwa wenyeji wa mashindayo yajayo ya mwaka 2028, jiji la Los Angeles la Marekani.

Soma pia: Seine-sational! Paris yatoa 'kwaheri' ya ushindi kwa Olimpiki

Tamasha la ufungaji lililodumu kwa masaa matatu katika uwanja wa Stade de France, lilishirikisha waigizaji na wasanii 270, akiwemo muimbaji maarufu wa Marekani Snoop Dogg katika sehemu ya ukabidhi kwa wenyeji wa michezo ijayo, jiji la Los Angeles.