1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais wa China kuitembelea Saudi Arabia siku ya Jumatano

6 Desemba 2022

Rais wa China Xi Jinping atafanya ziara ya siku tatu nchini Saudi Arabia wiki hii ambako atakutana kwa mazungumzo na mrithi wa kiti cha ufalme Mohammed Bin Salman.

https://p.dw.com/p/4KYcj
China Peking | Jiang Zemin Trauerfeier für Ex-Staats- und Parteichef | Xi Jinping
Picha: CCTV/AP/picture alliance

Shirika la habari la taifa nchini Saudi Arabia limesema hayo hii leo na kuongeza kwamba anatarajiwa kuwasili kesho Jumatano.

Rais wa China, pia atahudhuria mkutano wa kilele pamoja na watawala wa kifalme wanachama wa baraza la ushirikiano la nchi za Ghuba - GCC, pamoja pia na kuwa na mazungumzo na viongozi kutoka nchi nyingine za Mashariki ya Kati kuhusu kuimarisha uhusiano wa China na kanda hiyo unaoongezeka.

Ziara ya Xi Jingping nchini Saudi Arabia ni ya tatu nje ya nchi yake tangu kuzuka janga la Corona lakini pia inakuja katika wakati kuna mivutano mikubwa kati ya Saudi Arabia na Marekani kuhusu masuala kadhaa kuanzia sera ya nishati hadi usalama wa kikanda na haki za binadamu.