1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPeru

Rais wa China aahidi kushirikiana na utawala ujao wa Trump

17 Novemba 2024

Rais wa China Xi Jinping amesema nchi yake iko tayari kufanya kazi na utawala ujao wa Marekani chini ya rais mteule Donald Trump

https://p.dw.com/p/4n5IE
Peru | China Xi Jinping
Rais wa China Xi JinpingPicha: Fernando Vergara/AP Photo/picture alliance

Rais wa China Xi Jinping amesema nchi yake iko tayari kufanya hivyo ili kudumisha mawasiliano, kupanua ushirikiano na kudhibiti tofauti zilizopo kati ya nchi hizo kubwa kiuchumi duniani za China na Marekani. 

Soma Pia: Xi atoa wito wa maelewano na Marekani katika ujumbe wake kwa Trump

Xi aliyasema hayo katika mazungumzo yake na Rais wa Marekani anayemaliza muda wake, Joe Biden. Viongozi hao wamekutana mjini Lima kandoni mwa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano wa Kiuchumi la Asia-Pasifiki, (APEC), unaofanyika nchini Peru. Marais hao wa China na Marekani walizungumzia pia juu ya migogoro, uhalifu wa mtandaoni, biashara, Taiwan, Bahari ya Kusini ya China na Urusi, vita vya Ukraine na Korea Kaskazini.