1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Brazil kurejea tena katika kiti chake?

2 Septemba 2014

Wakati mbio za uchaguzi wa rais wa Oktoba 5 wa Brazil zikipata kasi, kumeonekana wimbi la watu lenye kumuunga mkono rais Dilma Roussef ambalo linatajwa kuwa kama ngao ya kumvusha rais huyo katika kinyang'anyiro hicho.

https://p.dw.com/p/1D5Rs
Brasilien Präsidentschaftswahl TV Debatte
Rais Dilma Roussef wa BrazilPicha: Reuters

Ingawa uchunguzi mpya wa kura za maoni unamuonesha Rais Dilma Roussef wa Brazil anakabiliwa na kibarua kigumu kuelekea uchaguzi wa hapo tarehe 5 Oktoba, kuna dalili pia kwamba wimbi jipya la ufuasi limezuka nyuma yake na huenda likamvusha salama kwenye kinyang'anyiro hicho akitetea kiti chake.

Uchunguzi wa kwanza wa maoni tangu kifo kilichotokana na ajali ya ndege wiki iliyopita cha mgombea urais wa chama cha kisoshalisti, Eduardo Campos, unamuonyesha Rais Rousseff katika wakati mgumu, na yumkini akaja akalazimika kuingia kwenye duru ya pili ya uchaguzi akipambana na mwanamazingira Marina Silvia.

Hali tete ya uchaguzi wa Brazil

Masoko ya fedha ya Brazil yaliimarika kutokana na uchunguzi huo, ambao unaonesha kwamba hakuna namna ambayo Roussef atashinda moja kwa moja kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi.

Brasilien / Dilma Rousseff und andere Präsidentschaftskandidaten
Rais wa Brazil akiwa katika mjadala wa kwenye TVPicha: Reuters

Wawekezaji wengi hawazipendi sera za Rousseff za mrengo wa kushoto na masoko kwa ujumla yameongezeka hivi karibuni na kuna kila dalili kwamba anaweza asishinde muhula wa pili.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taasisi ya uchunguzi wa maoni ya Datafolha, kuna ishara kwamba ufuasi wa Rousseff unakuja juu. Kiasi cha asilimia 38 wanasema serikali ya Roussef inafanya kazi nzuri, ikiwa ni ongezeko la asilimia 6 kutoka uchunguzi uliofanyika mwezi Julai. Huku wale wanaosema serikali hiyo ni mbaya nayo pia ikishuka kwa asilimia 6. Na haya yametokea wakati kiwango cha gharama za maisha kikishuka kwa kasi sana.

Hali ya uchumi Brazil

Muhula wake unakabiliwa na kukua taratibu kwa uchumi na kupanda kwa bei ya bidhaa kwa asilimi 6 kwa mwaka. Wapinzani wake wamekuwa wakimuandama kwa kuwa dhaifu kuruhusu kupanda kwa gharama za maisha licha ya mwezi Julai mwaka huu kushuhudiwa kushuka kwa gharama za tiketi za ndege na gharama za chakula kwa kipindi cha kombe la dunia ambapo Brazili walikuwa wenyeji.

Siku moja baada ya Campos kufariki katika ajali ya ndege Taasisi ya Datafolha ilianza kukusanya maoni ya uchuguzi na vyombo vya habari vya Brazil tangu wakati huo vimekuwa vikielezea sifa za Campos, mfanyabiashara rafiki wa zamani wa aliyekuwa mshindi wa tatu katika uchaguzi kwa asilimia 8 licha ya kuwa alikuwa akionekana kama mmoja wa vijana wanasiasa wa Brazili wenye uwezo wa kufanya kampeni kubwa ya uraisi mwaka 2018.

Siliva alikuwa mgombea mwenza wa Campos lakini alikuwa bora zaidi na alijulikana kitaifa, shukrani kwa kufahamika kwake kama mwanaharakati wa mazingira kwa nguvu yake na kumaliza kwa nafasi ya tatu kama mgombea uraisi katika uchaguzi wa mwaka 2010 na kuchukua asilimia 20.

Baadhi ya wachambuzi wanategemea kumuona Silva kwa kishindo katika uchunguzi wa maoni unaofanywa na taasisi ya kukusanya maoni ya Datafolha akifuata hisia za Campos aliyefariki. Inaonyesha Silvia atashinda kwa asilimia 21 ya kura katika mzunguko wa kwanza wa kura sawa na asilimia moja mbele dhidi ya mpinzani wake mwenye msimamo wa kati Seneta Aecio Neves ila alikuwa karibu na Rousseff ambaye alipata asilimia 36 matokeo hayo yakawa msaada kwa Rousseff na Neves katika raundi ya kwanza ambayo yalikuwa sawa na matokeo ya uchunguzi uliofanyika mwezi mmoja uliopita.

Matokeo hayo yanamaanisha ukuaji wa Silvia kwa asilimia13 ikilinganishwa na Campos aliyetokea kwa wapiga kura ambao awali walisita au waliokuwa wametekwa kutokana na maandamano ambao walikuwa kinyume na Rousseff na kuchukua kura kutoka kwa wagombea wakuu wawili.

Katika raundi ya pili jambo ambalo wachambuzi wanasema lipo sawa ni uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Datafolha unaonyesha Silvia ana asilimia 47 hadi asilimia 43 faida zaidi ya Rousseff, inamaanisha ni kuchoka kwa utaalamu toka utafiti ufike ukingoni na kuonyesha makosa ya kuongezeka au kupungua kwa asilimia 2.

Baadhi ya wachambuzi wanajiuliza swali Silvia atakuwa na uwezo wa kukua sasa katika uchunguzi ikizingatiwa muungano wake ni dhaifu kwa sasa nchi nzima ukilinganisha na kampeni ndogo na kugawanywa kwa muda wa bure wa television ya umma kutangazakama alivyofanya bila ya kutabirika.

Baadhi ya wanachama wa Campos kutoka chama cha kisoshalisti nchini Brazil wametilia shaka ahadi ya Silivia katika jukwaa la chama hali ambayo inaweza kufanya kuwa na baadhi ya mivutano juu ya kampeni ya uchaguzi Silvia ambae alikimbia kama mgombea wa chama cha kijani mwaka 2010 anatarajiwa kuzingatia yaliyoafikiwa.

Mwaka jana Silvia alijaribu kuanzisha chama kipya kilichojulikana kwa jina la Sustainability Network ila alishindwa kukisajili kwa kukosa saini kwa wakati kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2014. Chini ya saa 24 baadaye Silvia aliwashangaza wanasiasa wa Brazil na kuungwa mkono na Campos ambaye chama cha jukwaa kimetofautiana naye sana.

Neves na wanachama wa chama cha kisoshalisti wana nguvu nchi nzima kuliko muungano wa Silvia, lakini utafiti uliotolewa siku ya Jumatatu unaonyesha Neves msaada wake umelala katika tukio la kurudiwa baada ya kuvunjwa chunguzi nne ambazo zinamuonyesha alikuwa karibu na Rousseff.

Kwa mujibu wa taasisi ya kukusanya maoni ya datafolha kupitia uchunguzi walioufanya na kuwahoji watu 2,843 katika miji 176 siku ya Alhamisi na Ijumaa rais Rousseff anaongoza mbele ya Neves kwa asilimia 47 kati ya asilimia 39 ambazo zipo kwenye mstari katika kurudiwa kati yao.

Mwandishi: Zuhura Hussein
Mhariri: Josephat Charo