1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Brazil ajaribu kuyafufua mazungumzo ya biashara duniani

3 Agosti 2008
https://p.dw.com/p/EpkL

Brasilia:

Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil, ametangaza kwamba ameanza mashauriano na Marekani, China na India kuyaokoa mazungumzo ya biashara duniani. Rais Lula alisema alizungumzia suala hilo kwa simu na Rais George W.Bush wa Marekani na atazungumza na rais mwenzake wa China Hu Jintao wiki ijayo wakati wa michezo ya Olimpik mjini Beijing.

mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa biashara duniani yalivunjika mjini Geneva Jumanne iliopita, pale Marekani na India zilipokataa kuafikiana kuhusu suala la ruzuku kwa wakulima wa Marekani na ulaya. Rais Lula alisema anaamini majadiliano ya duru ya Doha kuhusu biashara yanaweza bado kukamilishwa baada ya uchaguzi nchini Marekani na India.