1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Brazil afunguliwa mashitaka ya rushwa

27 Juni 2017

Mwanasheria mkuu Brazil amemuhusisha kwa tuhuma za rushwa na kumfunguliwa mashtaka Rais wa taifa hilo Michael Termer, na kuwa rais wa kwanza aliye madarakani kutuhumiwa

https://p.dw.com/p/2fSWu
Brasilien Präsident Michel Temer in Brasilia
Rais Michel Temer wa BrazilPicha: picture-alliance/AP Photo/E. Peres

Hatua hiyo ya mwanasheria mkuu wa serikali Rodrigo Janot inatajwa kuwa mvutano mpya na mkubwa kabisa kutokea katika siku za hivi karibuni kati ya Temer na wanasheria ambayo wameifanya kesi hiyo ya rishwa kufikia katika kiwango cha juu kabisa. Kesi hiyo kwa hivi sasa itapelekwa kwa baraza la wawakilishi la Brazil, ambalo lazima liamue kama ina uhalali wa kuendelezwa.

Kama theluthi mbili ya wabunge wataamua kuwepo uhalali wa kiongozi huyo kushitakiwa, kinatakochofuata ni rais kusimamishwa kutumikia taifa hadi siku 180 wakati uchungzúzi wa kesi inayomkabilia ukiendeshwa. Kwa mujibu wa katiba ya Brazil, Spika wa Bunge Rodrigo Maia, ambae pia anatajwa kuwa mshirika wa karibu wa Rais Temer, atakuwa rais wa mpito.

Adaiwa kunyakua kitita cha dola 150,000

Rodrigo Janot
Mwanasheria Mkuu wa Brazil Rodrigo JanotPicha: picture alliance/dpa/A.Machado

Katika uamuzi wake Mwanasheria Mkuu Janot, amesema Temer katika kipindi cha Machi na Aprili mwaka huu alichukua rushwa ya kiasi cha dola 150,000, ambacho kilitolewewa na Joesly Batista, mwenyekiti wa zamani wa kampuni kubwa yenye kufanya shuguhuli za kufungasha nyama JBS. Janot alianzisha uchunguzi mwezi uliopita akijikita katika tuhuma za rushwa za rais huyo, kuzuia haki na kuwa sehemu ya uhalifu.

Pamoja na kuwepo kwa ushahidi unanafdaiwa kurekodiwa kutoka na vitendo hivyo vya rushwa kwa rais hiyo lakini mwenyewe ameibuka hadharani na kukanusha. Aidha amekwenda mbali na kusema hatojiuzulu wadhifa wake wa urais pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kumtaka afanye hivyo. Baada ya ripoti ya mwanasheria mkuu wa serikali ofisi ya rais jana jioni ilisema haiwezi kusema lolote kwa wakati huo.

Uamuzi wa Mwanasheria Mkuu Janot kutanguliza mbele tuhuma za rushwa tu, unaweza kuwa mkakati wa kulilazimisha baraza la wawaikilishi kuanza kushughulika na tuhuma hizo mapema kabla ya kuzingatia tuhuma nyinginezo. Washirikia wa rais Temer kwa wakati huo wapo katika njia ya panda ya kama je waendelee kumuunga mkono kiongozi huyo au waachane nae ili isije ikawagharimu katika uchaguzi mkuu  mwaka ujao.

Kurasa 64 za uamuzi wa mwanasheria mkuu, zinaonesha Rais Temer alivyochunguzwa pamoja na na vitendo vyake kama kiongozi wa juu kabisa nchini Brazil. Janot amesema rushwa  anayohusishwa nayo  kiongozi huyo inaweza kufikia kiasi cha dola milioni 12 katika kipindi cha miezi tisa.

Mwandishi: Sudi Mnette APE
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman