Rais wa Benki ya Dunia asema kundi la G7 limeshindwa majukumu yake
7 Oktoba 2008Katika hotuba yake aliyoitoa mjini Washington kabla ya mkutano wa wakuu wa nchi hizo saba tajiri, mwishoni mwa wiki hii, rais huyo wa Benki ya Dunia amesema kuwa mzozo wa fedha unaoikumba dunia hivi sasa ni ishara ya kwamba wigo wa ushirikiano unatakiwa kupanuliwa zaidi.
Amesema kuwa kundi hilo la mataifa tajiri yaani G7 limeshindwa kazi na kwamba linahitajika kundi lingine bora zaidi, kwa wakati tofauti.
Kundi hilo la G7 linaundwa na nchi za Marekani, Uingereza, Canada,Ufaransa, Ujerumani, Italia na Japan.
Pia Rais huyo wa Benki ya Dunia Roberts Zoellick ametangaza kuwa ataunda tume itakayoongozwa na Rais wa zamani wa Mexico Ernesto Zedillo kusaidia kuboresha muundo wa benki hiyo ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikidhibitiwa na Marekani.