Rais Talon wa Benin ashinda muhula mwengine madarakani
14 Aprili 2021Matangazo
Katika nafasi ya pili, mpinzani wake wa karibu, Alassane Soumanou wa chama cha FCBE, alipata asilimia 11.3 wakati kiongozi wa chama cha Democrats, Corentin Kohoue, akipata asilimia 2.4 ya kura.
Mahakama ya kikatiba inapaswa kuthibitisha matokeo hayo katika muda wa siku 10.
soma zaidi: Benin wafanya uchaguzi kukiwa na wasiwasi
Talon, mfanyabiashara wa zamani wa pamba, amekuwa madarakani tangu mwaka 2016. Katika utawala wake, ameshtumiwa kwa kukandamiza upinzani. Kwa mujibu wa taasisi ya mafunzo ya usalama nchini humo, ISS, ni kuwa karibu wanasiasa watano wa upinzani wamewekwa kizuizini.
Mwezi uliopita, mwanasiasa wa upinzani, Reckya Madougou, alikamatwa kwa mashtaka yanayohusiana na kuvuruga uchaguzi.