1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Afghanistan ziarani mjini Berlin

Oumilkher Hamidou11 Mei 2009

Rais Karzai aishukuru Ujerumani kwa kuisaidia nchi yake

https://p.dw.com/p/HniZ
Kansela Angela MerkelPicha: AP

Rais Hamid Karsai wa Afghanistan akiwa ziarani nchini Ujerumani,amekua na mazungumzo pamoja na kansela Angela Merkel mjini Berlin jana."Ujerumani itazidisha juhudi za kuwapatia mafunzo polisi na wanajeshi" ili kuimarisha utulivu nchini Afghanistan.Licha ya hali tete iliyoko nchini Afghanistan,kansela Angela Merkel anaamini watafanikiwa na amesifu ushirikiano wa dhati pamoja na Afghanistan.

Ujerumani inataka kuwajibika zaidi nchini Afghanistan.Amesema hayo kansela Angela Merkel baada ya mazungumzo pamoja na rais Hamid Karsai mjini Berlin.Ujerumani inapendelea kusaidia zaidi katika kuwapatia mafunzo polisi na jeshi,amesema kansela Angela Merkel:

""Nnahisi,na hili halistahiki kupuuzwa,tumepiga hatua muhimu mbele katika kipindi cha miezi na miaka iliyopita.Tunabidi tutilie maanani ukweli kwamba,katika mji mkuu Kabul,vikosi vya usalama vya Afghanistan ndivyo vinavvyobeba jukumu kubwa zaidi hivi sasa.Sawa kabisa kwamba ISAF wanalazimika bado kuwa nyuma yao ,lakini hali hii tulio nayo,hatukuifikiria miaka kama miwili hivi iliyopita."

Kansela Angela Merkel ameonyesha kuridhika pia na hakikisho la rais Hamid Karsai la kuifanyia marekebisho sheria inayobishwa ya ndowa kwa jamii ya wachache ya washiya,ambapo wanawake wanalazimishwa kulala mara kwa mara na waume zao.Mswaada wa megeuzi umeshawasilishwa bungeni,amesema rais Karsai aliyemshukuru kansela Angela Merkel kwa msaada wa Ujerumani kwa Afghanistan:

Hamid Karzai
Rais Hamid Karsai wa AfghanistanPicha: PA/dpa

"Nnakuamkieni na kukushukuruni kwa niaba ya wananchi wa Afghanistan kwa yote ambayo Ujerumani inatufanyia tangu miaka sabaa iliyopita,katika kuwapatia mafunzo askari polisi na wanajeshi wa Afghanistan,katika kuijenga upya na maenmdeleo ya Afghanistan,katika kutusaidia kuimarisha huduma za afya,elimu na shughuli za utawala.Nnashukuru kuwaona nyie,wanajeshi wenu na fedha za walipa kodi wenu,mmekuja kutusaidia ili kuimarisha mustakbal wa wananchi wa Afghanistan."

Rais Hamid Karsai na kansela Angela Merkel wamezungumzia pia wasi wasi uliopo kutokana na kuzidi kuwa mbaya hali nchini Pakistan ambako wataliban wanasonga mbele na mapigano yamepamba moto huku malaki ya watu wakiyapa kisogo maskani yao katika bonde la Swat.

Wakati huo huo rais Hamid Karsai amelaani vikali hujuma za vikosi vya nchi shirika dhidi ya raia nchini mwake.Akihojiwa na kituo cha televisheni cha ARD,rais Hamid Karsai amesema "vita dhidi ya ugaidi haviwezi kufanikiwa kwa kushambuliwa vijiji."

Mwandishi Marx Bettina(Berlin) / Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Josephat Charo