Rais Vladmir Putin amempokea rais wa Syria Bashar al-Assad
15 Machi 2023Matangazo
Kusaidia kurejesha uhusiano kati ya Uturuki na Syria kunatoa fursa kwa Kremlin kujiimarisha kidiplomasia, wakati ambapo Moscow inazidi kutengwa na mataifa ya magharibi baada ya kutuma vikosi vyake kuivamia Ukraine.
Mkutano huo unafuatia tangazo la wiki iliyopita la urejeshaji wa uhusiano kati ya mahasimu wa Mashariki ya Kati, Saudi Arabia na Iran, ulioratibiwa na China.
Soma pia:Putin ampongeza Xi kwa kuongezewa muhula wa tatu madarakani
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari kuwa mkutano kati ya Putin na Assad, aliewasili Moscow jana Jumanne jioni, unaangazia uhusiano kati ya mataifa hayo, lakini pia uhusiano kati ya Uturuki na Syria utagushwa kwa njia moja au nyingine.