Rais Uhuru aanza kutatua tatizo la ardhi Kenya
4 Septemba 2013Matangazo
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amekamilisha zoezi la utoaji wa hati za kumiliki ardhi zaidi ya 60,000 katika jimbo la Pwani hapo siku ya Jumatatu (02.09.2013). Zoezi hilo lilinuiwa kuanza hatua ya kwanza muhimu katika kulitafutia ufumbuzi tatizo sugu la ardhi nchini Kenya. Hata hivyo hatua ya rais Kenyatta imeibua hisia mbalimbali huku wengine wakiisifu na wengine wakiikosoa. Josephat Charo amezungumza na bwana Odenda Lumumba, wa Muungano wa Kitaifa wa masuala ya Ardhi, Natiaonal Land Alliance, na kwanza kumuuliza anazionaje juhudi za rais. Kuyasikiliza mahojiano haya bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Josephat Charo
Mhariri: Yusuf Saumu