Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi, mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (ECCAS) ndiye mpatanishi wa jumuiya hiyo katika mzozo wa Chad. Tshisekedi aliteuliwa katika mkutano wa Jumuiya hiyo uliomalizika Jumatatu na kuhudhuriwa na marais wanne miongoni mwa kumi na mmoja wa jumuiya hiyo. Jean Noël Ba-Mweze alituarifu kutoka huko Kinshasa.