Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania ipo mbioni katika jitihada za kuanzisha kiwanda cha kutengeneza chanjo ya COVID-19 na nyinginezo kwa lengo la kunusuru afya ya umma wa taifa hilo pamoja na kuokoa fedha nyingi ambazo taifa hilo linazitumia katika kununua chanjo. Kauli hiyo ameitoa katika mahojiano maalum aliyofanyiwa na Sudi Mnette.