Ni mwaka mmoja tangu serikali ya Kenya Kwanza ilipochukuwa hatamu za uongozi chini ya rais William Ruto. Wakenya wamekuwa wakilalamika kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha. Kenya Kwanza inashikilia imefanikiwa kuusawazisha uchumi kwa kulipunguza deni la taifa baada ya kuongeza mapato ya kodi. Ziadi juu ya hilo, Tatu Karema amezungumza na Martin Oloo Mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya.