Ruto atembelea kikosi cha polisi kilichoko nchini Haiti
22 Septemba 2024Rais wa Kenya William Ruto aliwasili nchini Haiti na kudai kwamba uwepo wa kikosi cha polisi kutoka Kenyakupambana na magenge ya kihalifu, kumeimarisha hali ya usalama nchini humo na kuruhusu raia waliokimbia makazi yao kurejea nyumbani.
Hata hivyo madai ya Ruto yanatofautiana na mtaalamu wa usalama wa Umoja wa Mataifa ambaye siku kadhaa zilizopita, alionya kwamba hali ya usalama katika taifa hilo imezidi kuwa mbaya, wakati magenge ya kihalifu yakizidi kupanua udhibiti wake katika taifa hilo la Karibiani. Kenya yaongeza maafisa 200 zaidi nchini HaitiMara baada ya kuwasili, Rais Ruto aliekelea moja kwa moja katika kambi ya kikosi cha polisi wa Kenya katika uwanja wa ndege na kukutana na maafisa waandamizi wa kikosi hicho, Haiti na Canada. Ruto ataelekea Marekani kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.