1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Putin aitaka Iran kutia maanani matakwa ya IAEA

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXYb

Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa mara nyingine tena ametoa mwito kwa Iran kusitisha mradi wake wa kurutubisha madini ya uranium.Wakati wa majadiliano yake pamoja na msuluhishi wa Iran Saeed Jalili mjini Moscow,Putin ametoa mwito kwa serikali ya Tehran kutia maanani matakwa ya Shirika la Nishati ya Atomu IAEA na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo Waziri wa Nje wa Urusi,Sergei Lavrov akijibu ripoti mpya ya Marekani kuhusu Iran amesema,kamwe hakujakuwepo ushahidi kuwa Tehran iliwahi kuwa na mradi wa kutengeneza silaha ya nyuklia.Amesema,ripoti ya Marekani ni kipengele cha kuamulia kama kuna haja ya kuweka vikwazo vipya dhidi ya Iran.Rais wa Iran Ahmedinejad amesema,ripoti ya wapelelezi ya Marekani ni tangazo la ushindi kwa Iran.