Rais Obama azungumzia milipuko ya mabomu Uganda
14 Julai 2010Matangazo
Rais Barack Obama wa Marekani akizungumzia milipuko miwili iliyotokea nchini Uganda, amesema makundi kama Al-Shabab na Al-Qaeda hayathamini maisha ya Waafrika na kwamba wanalenga bara la Afrika kuwa eneo la kuwaua watu wasio na hatia. Katika mahojiano na Shirika la habari la Afrika Kusini, Obama ambaye ana asili ya Kiafrika alisema matamshi wanayotoa makundi hayo yenye itikadi kali, yanaonyesha wazi maisha ya watu wa Afrika hayana thamani. Rais huyo wa Marekani aliongeza kuwa Al-Shabab na Al-Qaeda sasa wanalichukulia bara la Afrika kama jukwaa muafaka la kutekeleza itikadi zao kali, pamoja na kuwauawa watu wasio na hatia bila ya kujali athari za muda mrefu.