1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Obama athibitisha kifo cha kiongozi wa al Qaeda Osama bin Laden

2 Mei 2011

Kiongozi wa kundi la al Qaeda Osama bin Laden ameuwawa. Amethibitisha hayo rais wa Marekani Barack obama. Obama amesema operesheni ilifanywa siku ya Jumapili. Maiti yake imezikwa baharini.

https://p.dw.com/p/117U8
Osama bin LadenPicha: AP

Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza rasmi kwamba kiongozi wa al Qaeda Osama bin Laden ameuwawa na maiti yake iko mikononi mwa maafisa wa Marekani. Rais Obama ametangaza kifo cha Osama usiku wa Jumapili (01.05.2011) kutoa taarifa kamili kuhusiana na kuuwawa kwa kiongozi huyo baada ya juhudi ngumu zilizodumu miaka kadhaa.

"Marekani imefanya harakati ambapo Osama bin Laden, kiongozi wa al Qaeda na gaidi anayebeba dhamana kwa mauaji ya maelefu ya wanaume, wanawake na watoto," amesema rais Obama.

Rais Obama amesema bin Laden ameuwawa kwenye operesheni iliyowajumuisha maafisa wa Marekani na Pakistan waliokuwa na ushujaa na uwezo wa hali ya juu. Hakuna Wamarekani waliouwawa kwenye harakati hiyo na kwamba hatua muhimu zimechukuliwa kwa uangalifu mkubwa kuepusha vifo vya raia.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Prema Martin