1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Obama atarajiwa kuwasili Berlin

18 Juni 2013

Rais Barack Obama anatazamiwa kuwasili Berlin kwa ziara yake ya kwanza rasmi tangu alipokabidhiwa hatamu za uongozi nchini mwake.Kilele cha ziara hiyo ni hotuba katika uwanja wa lango la Brandenburg.

https://p.dw.com/p/18rs3
Rais Barack Obama ndani ya ndege yake ya Air Force OnePicha: Peter Muhly/AFP/Getty Images

Hatua za usalama zimeimarishwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita,uwanja wa Paris haupitiki tena ovyo ovyo.Kila pembe.vimewekwa vizuwizi na magari ya polisi.madereva wa magari ya kawaida na baskeli wanalazimika kupita njia nyengine,hata usafiri wa chini kwa chini na treni za masafa mafupi zimesitisha shughuli zake kuelekea eneo la kati la mji mkuu.

Hatua za usalama hazina mfano,maelfu ya polisi wa Ujerumani wamewekwa kila pembe,bila ya kuwataja wanajeshi wa usalama wa rais wa Marekani binafsi waliokuja na gari lao maalum kwa jina "The Beast" atakalopanda rais Obama atakapouzunguka mji mkuu Berlin.Hata katika mapaa ya nyumba zilizoko katika njia atakayopitia rais Obama vikosi vya usalama vimewekwa.Hata anga ya jiji la Berlin imefungwa hadi ndege ya rais wa Marekani Air Force One itakapotuwa.

Hotuba katika uwanja wa lango la Brandenburg

Obama in Berlin Sicherheitsvorkehrungen
Polisi anashika zamu katika uwanja wa lango la BrandenburgerPicha: Reuters

Rais Obama ameshafika mara tatu nchini Ujerumani,April mwaka 2009 mjini Baden Baden na Kehl,Juni 2009 mjini Buchenwald,Dresden na katika hospitali ya kijeshi ya Marekani huko Landstuhl katika jimbo la Rheinland Pfalz.Hii ni mara yake ya pili kuutembelea mji mkuu Berlin na ya kwanza kama rais wa Marekani.Kwa mara ya mwisho alifika Berlin mwaka 2008-wakati ule alikuwa mgombea kiti cha urais wa Marekani,kijana,mwenye fasaha na akishanagiriwa kama nyota inayong'ara ulimwenguni.Watu zaidi ya laki mbili walimiminika katika uwanja wa mhimili wa ushindi mjini Berlin kumshangiria,kumuona na kumsikiliza rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika.Kusema kweli wakati ule mgpombea huyo wa chama cha Democrats alitaka kuhutubu katika uwanja mashuhuri wa lango la Brandenburg,lakini kansela Angela Merkel alitaka kuwapa cheo hicho viongozi waliokwisha chaguliwa tu.

Kesho lakini,rais Barack Obama aliyeingia mhula wake wa pili madarakani na kuanza kupata mvi kichwani atahutubia katika uwanja wa lango la Brandenburger.Lakini kiu cha amiaka mitano na nusu hakiko tena.Atawaahutubia wageni zaidi ya elfu sita walioalikwa wakiwemo wanasiasa,mabalozi,wawakilishi wa kiuchumi na jamii na bibi mmoja wa Berlin aliyesoma shule moja na John F.Kennedy.Wajerumani watafuatilizia hotuba hiyo kupitia televisheni zao majumbani mwao.Hata sehemu kubwa ya waandishi habari watalazimika kufuatilizia matukio hayo nje kutokana na uhaba wa nafasi katika uwanja wa lango la Brandenburg.

Obama kipenzi cha umma Ujerumani

Obama und Merkel Freiheitsmedaille Archiv 2011
Rais Barack Obama na kansela Angela Merkel mnamo mwaka 2011Picha: picture-alliance/dpa

Haijulikani kama na safari hii pia malaki watateremka majiani kumlahiki rais huyo wa Marekani na mkewe Michelle na binti zao.Licha ya yote hayo lakini bado rais Obama anapendwa humu nchini:Asili mia 65 wanasema wangempigia kura mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel wangetakiwa wafanye hivyo,na asili mia 41 wengine wanahisi rais Obama amefanikiwa zaidi kuliko kansela Angela Merkel.

Mwandishi:Marx Bettina/Hamidou Oummilkheir

Mhariri :Mohammed Abdul-Rahman