Rais Mugabe wa Zimbabwe hajaalikuwa kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola ( Commonwealth):
26 Novemba 2003Matangazo
ABUJA: Rais OLUSEGUN OBASANJO wa Nigeria ameshikamana na wanaompinga rais Robert Mugabe wa Zimbabwe. Mugabe hajapelekewa mualiko wa kushiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth) mwezi ujao nchini Nigeria, - alitamka OBASANJO. Uongozi wa Zimbabwe haujaweza kufikia uwelewano wa kuridhisha wakati wa ukizungumza na wapinzani wake nchini. Jumuiya ya Kimataifa iliigomea Zimbabwe kufuatia matokeo yanayobishwa ya uchaguzi wa rais, Machi mwaka 2002. Kadhalika Muungano wa Ulaya ulitangaza vikwazo dhidi ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa makisio ya wachunguzi wa kimataifa, Mugabe ameshinda kwa matumizi ya mabavu, vitisho dhidi ya upinzani na ulaghai uchaguzini.