1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Mugabe apata changamoto mpya

6 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D39o

HARARE:

Mwanachama mwandamizi wa chama tawala cha Zimbabwe,ZANU-PF amesema, anapanga kutoa changamoto kwa Rais Robert Mugabe katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanywa mwezi Machi.Aliyekuwa Waziri wa Fedha Simba Makoni amesema,ameamua kuwa mgombea huru baada ya kushauriana na wanachama wenzake kote nchini.Inasemekana kuwa hii ni changamoto kali kabisa kwa uongozi wa Mugabe tangu zaidi ya miaka 20.

Wakati huo huo,makundi mawili hasimu katika chama kikuu cha upinzani cha MDC yameshindwa kuafikiana nani atakaetoa changamoto kwa Mugabe.Wakosoaji wa Robert Mugabe,wanamlaumu kiongozi huyo kwa uchumi uliozorota nchini Zimbabwe.Rais Mugabe alie na miaka 83 anatawala tangu mwaka 1980.