SiasaTaiwan
Rais mteule wa Taiwan asifu mahusiano na Marekani
15 Januari 2024Matangazo
Amesema hayo wakati akiukaribisha ujumbe wa Marekani Jumatatu, ambao China imesema inaupinga vikali.
Wakati Taiwan haitambuliwi kidiplomasia na Marekani, Washington ni mshirikka na muuzaji wake mkuu wa silaha.
Kisiwa hicho kimepoteza mmoja wa washirika wake wachache rasmi wa kidiplomasia, baada ya taifa la Bahari ya Pasifiki Nauru kutangaza kuwa inasitisha mahusiano na kuanzisha mahusiano na Beijing.
Uamuzi huo wa Nauru, unaojiri siku chache tu baada ya uchaguzi wa rais wa Taiwan, una maana ni mataifa 12 pekee yanayoitambua rasmi Taiwan, ambayo Beijing inadai ni sehemu ya himaya yake.
Tangazo la Nauru limeifunika ziara ya ujumbe usio rasmi uliotumwa na utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden kumpongeza Lai.