1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Mbeki yuko Zimbabwe kwa mazungumzo ya usuluhishi

Mohamed Dahman10 Agosti 2008

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini yuko katika mji mkuu wa Zimbabawe Harare kwa mazungumzo ya usuluhishi wa kushirikiana madaraka kati ya upinzani na viongozi wa serikali.

https://p.dw.com/p/Etr2
Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini msuluhishi wa mgogoro wa ZimbabwePicha: AP

Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai amewasili kwenye hoteli moja ya Harare leo hii kwa mazungumzo hayo na Rais Robert Mugabe huku kukiweko dalili kwamba makubaliano yamefikiwa.

Tsvangirai ambaye hakuandamana na maafisa wengine kutoka chama chake cha MDC hakuzungumza na vyombo vya habari.

Mugabe pia anatazamiwa kukutana na kiongozi wa kundi lililojitenga la MDC Arthur Mutambara ambaye amesema leo hii kwamba makubaliano ya kushirikiana madaraka tayari yamefikiwa.

Kuna repoti kwamba vyama hivyo vimekubaliana kimsingi kumchaguwa kiongozi wa upinzani Tsvangirai katika wadhifa mpya ulioanzishwa wa waziri mkuu.

Mazungumzo hayo yanakusudia kutatuwa mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo ambao umechochewa kutokana na matokeo ya uchaguzi wa urais yaliozusha utata mapema mwaka huu.