1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAIS MBEKI AITETEA ZIMBABWE

22 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFbu

TEHERAN:

Kumetokea mtetemeko wa ardhi kusini-mashariki mwa Iran mapema hii leo ambamo watu si chini ya 190 wameuwawa na wengine 1000 wamejeruhiwa.Zilzala hiyo imetokea kandoni mwa mji wa ZARAND na katika mkoa wa KERMAN,km 700 kusini mashariki mwa mji mkuu Teheran.

Zilzala hii imefikia kipimo cha 6.4 cha RICHTER.

BRUSSELS:

Rais George Bush wa Marekani amewasili leo katika makao makuu ya NATO-shirika la ulinzi la magharibi mjini Brussels kwa mkutano wa kilele na wanachma 26 wa jumuiya hiyo.Mkutano wake wa kwanza ulipangwa na rais wa Ukrain,Viktor Yuschchenko.Baadae atakua na mkutano na Umoja wa Ulaya uliogawika juu ya uvamizi wa Marekani nchini Irak.

Awali, rais Bush alifungua kinywa kwa chai ya asubuhi na waziri mkuu wa Uingereza ,Tony Blair.Baadae Bw.Blair alisema njia ya kuleta ufumbuzi wa amani wa mgogoro wa Mashariki ya kati sasa imenyoka na rais Bush atatia mkazo zaidi.

RIYADH:

Waziri wa nje wa Saudi Arabia,mwanamfalme Saud al-Feisal amesema nchi zisifyatuke tu kuilaumu Syria kuhusika na mauaji ya waziri-mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafik Hariri.

Waziri huyo wa Saudia alipinga pia mwioto wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa juu ya kifo cha Hariri.Alisema, Lebanon iachiwe ifanye uchunguzi wake binafsi.

Viongozi wa Upinzani nchini Lebanon wamekuwa wakiinyoshe kidole syria kuhusika na mauaji ya Bw.Hariri.

Marehemu alikua na usuhuba mkubwa na mfalme wa saudi Arabia na alikua na uraia pia wa Saudia mbali na ule wa Lebanon.

JOHANNESBERG:

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini ameituhumu Marekani kwa kuirodhesha Zimbabwe kuwa mojawapo ya nguzo za udikteta ulimwenguni.Mbeki alisema nchi yake ya Afrika Kusini yaweza kusaidia kufamnyika kwa uchaguzi huru nchini Zimbabwe mwezi ujao.

Katika mazungumzo na gazeti la FINANCIAL TIMES la London,rais Mbeki hatua ya Marekani ya kuiorodhesha Zimbabwe miongoni mwa mataifa ya kidikteta kumeharibu siasa yake inayodai kupalilia uhuru ulimwenguni.