Rais Lula atoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa Haiti
29 Februari 2024Matangazo
Lula ameyasema haya katika mkutano wa kilele wa mataifa ya Caribbean ambapo kulifikiwa makubaliano ya kisiasa kuhusiana na nchi hiyo iliyo kwenye mgogoro.
Rais huyo wa Brazil amesema hatua za haraka zinastahili kuchukuliwa ili kuwaondolea mateso raia wa nchi hiyo.
Hapo juzi Jumanne, Umoja wa Mataifa ulitoa wito wa dola milioni 674 kwa ajili ya miradi ya kiutu nchini Haiti ambako asilimia 45 ya idadi jumla ya watu nchini humo, hawana usalama wa chakula.
Umoja wa Mataifa unasema, mwezi Januari pekee, zaidi ya watu 1,100 waliuwawa, kujeruhiwa au kutekwa nyara.
Kwengineko Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ariel Henry amesema yuko tayari kuunda serikali ya muungano na upinzani hadi pale uchaguzi utakapofanyika.