1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Rais Kagame afanya mabadiliko makubwa ndani ya jeshi

7 Juni 2023

Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mabadiliko makubwa ndani ya jeshi la nchi hiyo siku moja baada ya kuteua waziri mpya wa ulinzi, mkuu wa majeshi na kiongozi wa idara ya usalama wa taifa.

https://p.dw.com/p/4SHyg
Mosambik | Besuch Filipe Nyusi und Paul Kagame in der Provinz Cabo Delgado
Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa Pemba katika mkoa wa Cabo Delgado.Picha: Simon Wohlfahrt/AFP/Getty Images

Katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa leo makamanda wawili waandamizi, maafisa 14, na watu wengine 200 wenye nafasi tofauti ndani ya jeshi wamefutwa kazi.

Hakuna sababu iliyotolewa juu ya maamuzi hayo ya ghafla.

Hapo jana Rais Kagame alitangaza kumteua Juvenal Marizamundakuwa waziri mpya wa ulinzi akichukua nafasi ya Albert Murasira aliyehudumu kwenye wadhifa huo tangu mwaka 2018.

Pia amemteua Mubarak Muganga kuwa mkuu wa majeshi na Jean Bosco Ntibitura kuongoza idara ya usalama wa ndani wa taifa.

Mabadiliko hayo yamewagusa pia makamanda wawili waliokuwa wakiongoza kikosi cha Rwanda kilichotumwa nchini Msumbiji kupambana na makundi ya wapiganaji wa itikadi kali.