Rais Kabila atangazwa mshindi wa uchaguzi DRC
10 Desemba 2011
Tume hiyo imesema kuwa mgombea wa karibu ya Kabila, kiongozi wa upinzani Etienne Tshsekedi , amepata asilimia 32 ya kura. Watu waliojitokeza kupiga kura katika nchi hiyo kubwa barani Afrika ni asilimia 59.
Tshisekedi amekataa matokeo hayo na kujitangaza kuwa rais mteule. Mahakama kuu katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo inapaswa hadi tarehe 17 mwezi huu kusikiliza rufaa za uchaguzi huo. Wakati matokeo yakitangazwa mjini Kinshasa jana Ijumaa, waungaji mkono wa rais Kabila walishangiria lakini wafuasi wa Tshisekedi wameeleza kuwa na hali ya wasi wasi. Ghasia wakati wa uchaguzi wa hapo Novemba 28 zimesababisha watu 18 kuuawa na kusababisha baadhi ya wakaazi kuikimbia nchi hiyo. Wachunguzi wa kimataifa wamesema kuwa uchaguzi huo umekumbwa na mapungufu kadha lakini wameshindwa kuuita wa udanganyifu. Matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge yanatarajiwa ifikapo katikati ya mwezi wa Januari. Rais ataapishwa Desemba 20.