1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Joe Biden atoa hotuba yake kuhusu hali ya taifa

Sylvia Mwehozi
8 Machi 2024

Rais wa Marekani Joe Biden ametoa hotuba yake ya mwisho kuhusu hali ya taifa ya Marekani kabla ya uchaguzi wa rais wa mwaka huu. Biden ameonya kwamba misingi ya demokrasia imeshambuliwa ndani na nje ya mipaka ya nchi.

https://p.dw.com/p/4dI9r
Joe Biden
Rais Joe Biden wa Marekani akitoa hotuba kuhusu hali ya taifaPicha: Kevin Lamarque/REUTERS

Rais wa Marekani Joe Biden ametoa hotuba yake ya mwisho kuhusu hali ya taifa ya Marekani kabla ya uchaguzi wa rais wa mwaka huu. Katika hotuba yake anayoitoa ndani ya bunge, Biden ameonya kwamba misingi ya demokrasia imeshambuliwa ndani na nje ya mipaka ya nchi hiyo.

Hotuba ya mwaka jana: Biden kutoa hotuba ya hali ya taifa

Biden alikuwa akirejelea vita vya Rais Vladimir Putin wa Urusi nchini Ukraine, akisisitiza kwamba hatoishia tu Ukraine. Amesema Ukraine inao uwezo wa kumsimamisha Putin kama itapatiwa silaha inazozihitaji kuweza kujilnda.

Kwenye hotuba yake hiyo katika majengo ya bunge ya Capitol Hill, Biden amekanusha uwepo wa wanajeshi wa Kimarekani nchini Ukraine, akisema amedhamiria kuendeleza msimamo huo.

Aidha pia, Biden hakusita kumshambulia Donald Trump kwamba alikusudia kuzima ukweli kuhusu uasi wa januari 6 na kuongeza kwamba ghasia hizo zilikuwa ni tishio kubwa kwa demokrasia ya Marekani tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe.