1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Xi Jinping akutana na rais wa Zambia Hakainde Hichilema

15 Septemba 2023

Rais wa China Xi Jinping amekutana na mwenzake wa Zambia Hakainde Hichilema mjini Beijing, wakati taifa hilo la Afrika lililoelemewa na madeni likijitahidi kuimarisha uhusiano wake na China.

https://p.dw.com/p/4WNBE
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema alipozuru kanisa katika eneo la makaburi ya halaiki kwenye mji wa Bucha nchini Ukraine, Juni 16,2023
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema alipozuru kanisa katika eneo la makaburi ya halaiki kwenye mji wa Bucha nchini Ukraine, Juni 16,2023Picha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Taarifa iliyotolewa na shirika la habari la serikali ya China CCTV, imesema rais Xi amesema urafiki wa China na Zambia umestahamili kile alichokiita "dhoruba na mabadiliko ya kimataifa"

Kiongozi huyo wa China ameeleza kuwa, taifa hilo linalenga kuugeuza urafiki huo kuwa, ushirikiano wa mafanikio kati ya nchi hizo mbili kuelekea enzi mpya.

China pia ina hisa kubwa katika sekta ya madini nchini Zambia.

Beijing imezindua miradi mikubwa ya miundombinu ikiwa ni pamoja na viwanja vya ndege, barabara na miradi ya nishari hata kabla ya Hichilema kuingia madarakani mwaka 2021.

Hata hivyo, Hichilema anaonekana kuwa na uhusiano wa karibu na Marekani huku Rais Joe Biden akimsifu kwa kujitolea kwake katika kuimarisha demokrasia.