Rais Bush apitisha viwakzo vya kiuchumi dhidi ya PKK
31 Mei 2008WASHINGTON
Rais Goerge W Bush wa marekani ametangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya waasi wa kikurdi wa kundi la PKK nchini Uturuki.Rais Bush ametumia sheria ya Marekani inayohusu biashara ya mihadarati kuweka vikwazo hivyo ambavyo vinawazuia waasi hao wa PKK kuingia katika mfumo wa fedha wa Marekani pamoja na kuzuia biashara yoyote itakayoyahusisha makampuni ya marekani na watu binafsi.
Viokwazo kama hivyo pia vimewekwa dhidi ya kundi la Mafia la Italia linalojulikana kama Ndrangheta pamoja na mtandao wa biashara za mihadarati wa Mexico Uturuki inaamini kwamba kundi hilo la PKK linatumia biashra ya mihadarati kufadhili shughuli zake.Uturuki,Marekani na Umoja wa Ulaya wanalitaja Kundi hilo la PKK kuwa la magaidi.Zaidi ya watu elfu 30 wameuwawa tangu kunid hilo lilipoanza harakati zake za kutaka kujitenga na Uturuki mwaka 1984.