Rais Bush akaribisha sheria mpya nchini Iraq
13 Januari 2008BAHRAIN:
Rais George kabla ya kuondoka Bahrain amekaribisha sheria mpya nchini Iraq ambayo itawakubalia baadhi ya wanachama wa chama cha Saddam Hussein cha Baathi kurejelea maisha ya kawaida.
Rais Bush amesema kuwa sheria hiyo ni hatua muhimu kuelekea maridhiano ya kitaifa nchini Iraq. Maelfu ya wanachama cha Baathi walifutwa kazi za serikali na mtawala wa Marekani baada ya uvamizi
Uliongozwa na Marekanimwaka 2003.Wengi wanamini kuwa hilo lizusha mgawanyiko mkubwa nchini humo,ambao umetia chumvi harakati za chini kwa chini.Sheria mpya ya uwajibikaji na sheria imepasishwa bila kupingwa na bunge la Iraq hiyo jana.Pia Bush ametumia ziara yake huko kuwashukuru viongozi wa Bahrain kwa kukubali kikosi cha wana maji cha Marekani cha tano kutia nanga huko.