Rais Aristide aihama Haiti:
29 Februari 2004Matangazo
PORT-AU-PRINCE: Kwa sababu ya kuendelea mgogoro wa ndani nchini Haiti Rais Jean-Bertrand Aristide yuko njiani kwenda uhamishoni. Msemaji wa upinzani alisema Rais Aristide yu njiani kwendea Jamhuri ya Doninican. Rais huyo wa Haiti ana niya ya kuomba hifadhi ya siasa Morokko, Taiwan au Panama, alisema. Ikulu ya Marekani mjini Washington imethibitisha safari hiyo ya Rais Aristide, kama vile lilivyoripoti Shirika la Utangazaji la Kimarekani CNN. Tangu waanzishe harakati zao za kupigana hapo mwanzoni mwa Februari wakitokea Kaskazini, waasi wamekwisha dhibiti zaidi ya nusu ya ardhi ya Haiti. Waasi hao ni mwungano wa makundi ya upinzani na wanajeshi wa zamani wa jeshi lililouzuliwa 1995. Zaidi ya watu 100 wamekwisha uawa katika mapigano hayo yanayoendelea nchini Haiti.