Kiongozi wa upinzani Kenya, Raila Odinga ametangaza kuanza rasmi maandamano ya kitaifa dhidi ya serikali kuu ya Kenya Kwanza, ambayo inadaiwa kuwa haramu. Je matarajio ya Odinga ni yepi na jitihada zake zitafanikisha matakwa yake? Grace Kabogo amezungumza na Martin Oloo, mchambuzi wa masuala ya siasa kutoka Nairobi.