1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia milioni 400 wa Ulaya waendelea kupiga kura

Sylvia Mwehozi
8 Juni 2024

Takriban raia milioni 400 wa Umoja wa Ulaya wanaendelea na zoezi la upigaji kura leo, kuwachagua wajumbe wa Bunge la Ulaya.

https://p.dw.com/p/4goc1
Uchaguzi Ulaya 2024 | Upigaji kura Barcelona
Raia wa Italia akipiga kura mjini BarcelonaPicha: picture alliance / Sipa USA

Uchaguzi huu ni mojawapo ya matukio makubwa ya kidemokrasia duniani.

Vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia vinatafuta kupata uungwaji mkono zaidi katikati mwa ongezeko la gharama za maisha na kutoridhika kwa wakulima. Vita vya Gaza na Ukraine pia ni miongoni mwa masuala yanayojadiliwa mno.

Uchaguzi wa Bunge la Ulaya  hufanyika kila baada ya miaka mitano katika jumuiya hiyo yenye wanachama 27.

Uchaguzi huo ulianza Alhamisi wiki hii nchini Uholanzi na utakamilika siku ya Jumapili, wakati nchi nyingi zitakapokamilisha zoezi la uchaguzi. Matokeo ya awali yataanza kutolewa jioni baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa katika nchi zote wanachama.