Raia wa Venezuela waandamana kuunga mkono upinzani
31 Julai 2024Matangazo
Waandamanaji hao mjini Caracas, waliimba wakisema wanataka uhuru huku viongozi wa kisiasa wakisisitiza kwamba walipata kura nyingi za kuhakikishia ushindi.
Miito ya kimataifa imetolewa kwa Baraza la Taifa la Uchaguzi (CNE) linaloegemea upande wa Maduro kutoa maelezo ya kina ya kila hatua kuthibitishia ushindi wa Maduro.
Rais wa Venezuela aamuru jeshi na polisi kushika doria nchi nzima
Maduro amesema upinzani utawajibishwa kwa ghasia za uhalifu, kusababisha majeruhi, vifo na uharibifu unaohusishwa na maandamano hayo.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Foro Penal, limesema takriban watu 11, wawili kati yao wakiwa watoto, walifariki katika kile ambacho mkuu wa shirika hilo Alfredo Romero amekielezea kuwa "mgogoro wa haki za binadamu''.