1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Raia wa Uturuki wanaoishi nje ya nchi waanza kupiga kura

20 Mei 2023

Raia wa Uturuki wanaoishi kwenye mataifa ya kigeni, wameanza kupiga kura leo katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wiki moja baada ya kushindwa kupatikana kwa mshindi wa wazi katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4Rc8d
Waturuki wakipiga kura mjini Berlin
Waturuki wakipiga kura mjini Berlin Picha: Michael Kuenne/PRESSCOV/ZUMA/picture alliance

Kwenye uchaguzi huo ambao nchini Uturuki utarudiwa Mei 28, Rais wa sasa Recep Tayyip Erdogan anawania kutetea kiti chake dhidi ya mpinzani wake mkuu Kemal Kilicdaroglu. Takribani Waturuki milioni 3.4 waishio nje ya taifa hilo wanakidhi vigezo vya kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Uchaguzi wa duru ya kwanza ulifanyika Jumapili iliyopita na Erdogan alipata chini ya asilimia 50% ya kura zinazohitajika ili kushinda kiti cha Urais nchini Uturuki.