Raia wa Tanzania aachiwa huru baada ya kuzuiliwa nchini Afghanistan kwa madai kuhusika na ugaidi.
1 Septemba 2008Matangazo
Mwanamume huyo aliyekuwa mvuvi alikuwa akifanya biashara yake katika maeneo ya Somalia na Visiwani humo alipokamatwa.Alizuiliwa kwa kipindi cha miaka minne nchini Afghanistan chini ya ulinzi mkali na kuteswa kwenye jela ya kituo cha jeshi la Marekani cha Baghram.Baada ya hapo aliruhusiwa kurudi nyumbani na kusaidiwa na Shirika la Msaada la msalaba mwekundu Redcross.
Mwandishi wetu wa Zanzibar Salma Said alikutana na Suleiman Abdala Salim punde alipowasili visiwani.Anaanza na kueleza jinsi alivyokamatwa nchini Somalia