1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Somaliland wapiga kura kuwachagua wabunge

31 Mei 2021

Raia wa Somaliland wanashiriki uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa jambo linaloonyesha maendeleo katika eneo hilo la Somalia lenye utawala wa ndani

https://p.dw.com/p/3uDK7
Somaliland Wahlen
Picha: Getty Images/AFP

Zaidi ya watu milioni moja kati ya milioni 4 wa Somaliland wamejiandikisha kama wapiga kura.

Waangalizi wa uchaguzi wakiwemo wanasiasa wakuu kutoka sehemu zengine za Afrika wamealikwa kuangalia jinsi zoezi hilo litakavyoendeshwa.

soma zaidi: HRW yaishutumu Somaliland kwa kukandamiza uhuru wa kutoa maoni

Somaliland ilijitenga kutoka Somalia mwaka 1991 baada ya nchi hiyo kutumbukia kwenye mapigano yaliyoongozwa na wababe wa kivita.

Eneo hilo kwa miaka mingi limekuwa na amani kinyume na sehemu zengine za nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.