Raia wa Finland wapiga kura ya urais
28 Januari 2024Wagombea tisa wanawania nafasi hiyo ili kujaza nafasi ya Rais Sauli Niinisto, mwenye miaka 75 anayetakiwa kuondoka madarakani baada ya kukaa madarakani kwa mihula miwili.
Soma pia: Finland nchi yenye furaha zaidi duniani
Takriban raia milioni 4.5 wenye sifa, wanatarajiwa kupiga kura. Awali kura za maoni zilionesha kuwa mgombea wachama cha kihafidhina Alexander Stubb, na waziri wa zamani wa mambo ya kigeni Pekka Haavisto chama cha kijani wanapewa nafasi kubwa kwenye kinyang'anyiro hicho.
Soma pia: Putin aitisha Finland kufuatia hatua yake ya kujiunga na jumuiya ya kujihami ya NATO
Matokeo ya awali yanatarajiwa kufahamika Jumapili jioni. Ikiwa hakuna mgombea atakayepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo, wagombea wawili wwaliopata kura nyingi zaidi wataingia katika awamu ya pili ndani ya wiki mbili.