1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani ya Kusini

Raia wa Ecuador wanajiandaa kwa uchaguzi wa marudio.

21 Agosti 2023

Wapiga kura nchini Ecuador wanajiandaa kwa uchaguzi wa marudio mwezi Oktoba baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais hapo jana kushindwa kutoa ushindi wa moja kwa moja kwa wagombea.

https://p.dw.com/p/4VOY1
Ecuador, Quito | Präsidentschaftskandidatin Luisa Gonzalez
Picha: Franklin Jacome/Getty Images

Mgombea kutoka upande wa kambi ya siasa za mrengo wa kushoto, Luisa Gonzalez, ambaye yuko karibu na rais wa zamani, Rafael Correa, aliongoza kwa asilimia 33 ya kura baada ya asilimia 80 ya kura kuhesabiwa hapo jana. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Diana Atamaint, amesema matokeo ya uchaguzi huo yameonesha hakuna mgombea aliyevuka kiunzi cha kupata ushindi wa moja kwa moja baada ya zoezi hilo lililofanyika chini ya ulinzi mkali.Gonzalez huenda akapambana na Daniel Noboa aliyepata asilimia 24 katika uchaguzi wa marudio Oktoba 15. Ecuador inakabiliana na hali ngumu ya usalama kufuatia vurugu za magenge ya biashara ya mihadharati.