Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekimbilia nchini Uganda wakihofia usalama wao kufuatia mapigano makali kati ya majeshi ya nchi hiyo na kundi la waasi wa M23. Kulingana na raia hao, jeshi la taifa la Kongo, FARDC limekuwa likijaribu kukomboa maeneo yanayodhibitiwa na M23 Mashariki mwa nchi sehemu za Bukanza. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu Lubega Emmanuel.