Raia wa Angola wapiga kura katika kinyang'anyiro kikali
24 Agosti 2022Matangazo
Taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta limekuwa chini ya utawala wa chama cha MPLA kwa karibu miongo mitano.
Chama hicho tawala kinapigiwa upatu, ijapokuwa pengo ni dogo mno kati yake na chama cha upinzani cha UNITA ambacho huenda kikabadilisha mahusiano kati ya taifa hilo na mataifa makubwa ulimwenguni, lakini kikitarajiwa kupunguza ushirikiano na Urusi.
Tangu kupata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975 Angola imekuwa ikitawaliwa na chama cha MPLA, kinachoongozwa na rais Joao Lorenco, aliyechukua madaraka mwaka 2017.
Kufuatia mchuano huo kuwa mkali, upinzani umewataka wafuasi wao kubaki karibu na vituo baada ya kupiga kura ili kupunguza uwezekano wa kufanyika udanganyifu.