Raia hatarini zaidi katika mji wa Mosul
2 Novemba 2016Baraza la wakimbizi la Norway linalowashughulikia Wairaq ambao wamegeuka wakimbizi wa ndani limesema kuwa karibu Wairaq 18,000 wameyakimbia makaazi yao tangu kuanza kwa oparesheni ya kijeshi inayolenga kuutwaa mji wa Mosul ambayo ilianza karibu wiki mbili zilizopita, kiongozi wa baraza hilo nchini Iraq Wolfgang Gressman amesema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo sasa wamejitayarisha kwa hali mbaya zaidi ambayo inaweza kutokeza.
Idadi ya watu walio katika hatari inaweza kuongezeka zaidi katika siku zijazo kutokana na mashambulizi kuongezeka, hii ni baada ya majeshi kutangaza kuwa majeshi maalumu yamefanikiwa kupenya katika eneo hilo siku ya Jumanne.
Katika mashambulizi ya kuukomboa mji wa Mosul majeshi ya Iraq kwa mara ya kwanza katika miaka miwili jana siku ya jumanne yalifanikiwa kuingia eneo la mashariki katika miji ya Gogjal na Karama ilyomo ndani ya Mosul.
Hali mbaya ya hewa yasitisha mashambulizi
Kiongozi wa vikosi maalumu vya Iraq amesema majeshi yake yamejidhatiti na kushika nafasi zao katika eneo la mashariki mwa Mosul licha ya kuwa hali mbaya ya hewa inadhoofisha operesheni kuelekea wapiganaji wa kundi la IS katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini humo.
Brigedia Generali Haider Fadhil amesema hakuna mpango wowote wa kupiga hatua kuelekea mji huo ambazo zimepangwa kufanyika leo Jumatano kutokana na kuwepo kwa hali mbaya ya hewa kama vile unyevunyevu na mawingu yenye giza hali ambayo inasababisha ugumu wa kuendelea kwa oparesheni za ndege
Msemaji katika ofisi ya tume ya haki za binadamu OHCHR Ravina Shamdasani amesisitiza msimamo wa kuwalinda raia na kusema kuwa
"Tunakaribisha kauli ambayo imetolewa na serikali ya Iraq kuwa ulinzi wa raia litakuwa ni jambo la kuzingaziwa wakati majeshi yakiendelea na mikakati ya kuutwa mji wa Mosul na tunahitaji kuendelea kuwakumbusha kuhusu ukatili ambao unafanywa na IS, hatua za kulipiza mashambulizi zinafanyika huko, lakini tunawakumbusha tena pande zote kuwa ukiachilia mbali ukatili unaofanywa na IS kuna jukumu ambalo liko chini ya sheria za kimataifa za kulinda raia"
Katika eneo la Gogjali karibu na mji wa Mosul hakujasikika milio ya risasi pamoja na kuwa kumekuwepo na milio ya hapa na pale wakati ambao majeshi huripua mizinga kuelekea upande wa IS, kusitishwa kwa mashambulizi,baada ya siku jana majeshi ya Iraq kuingia kwa mara ya kwanza katika mji huo kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili huku yakijiandaa kwa mashambilizi ambayo yanatarajiwa kuchukua wiki ama miezi kadhaa.
Mwandishi: Celina Mwakabwale/AP/AFP
Mhariri:Iddi Ssessanga