Raia 25 wa Senegal waokolewa baharini na 102 wamepotea wakijaribu kuingia Uhispania kwa magendo.
17 Desemba 2006Matangazo
Dakar:
Wavuvi huko Senegal wamewaokoa raia 25 wa nchi hiyo waliokuwa wanasafiri na kutaka kuhamia Uhispania kwa magendo, lakini wengine 102 bado wamepotea baharini. Wale walionusirika walisema watu 130 walianza safari yao wiki mbili zilizopita wakiwa ndani ya boti ya mbao, wakitokea Bolongne, kusini mwa Senegal, wakielekea visiwa vya Canary vya Uhispania, nje ya mwambao wa Afrika Magharibi. Wale waliookolewa walichukuliwa jana hadi katika hospitali ya kimkoa katika mji wa Saint-Louis, huko Senegal.