RABAT: Hali ya tahadhari yaimarishwa Morocco
7 Julai 2007Matangazo
Hali ya tahadhari dhidi ya ugaidi imepandishwa kiwango cha juu kabisa nchini Morocco.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani mjini Rabat,hatua hiyo imechukuliwa kufuatia „habari za kuaminika“ kuhusika na kitisho cha kigaidi.Vikosi vya usalama pia vimewekwa katika hali ya tahadhari na ukaguzi umeimarishwa kote nchini.Ziara ya Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa,iliyopangwa kufanywa nchini Morocco juma lijalo,imeahirishwa hadi mwezi wa Oktoba.