1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

QUITO :Duru ya pili ya uchaguzi wa rais-Ecuador

26 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpC

Wapiga kura nchini Ecuador hii leo wanapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais.Mgombea wa chama cha mrengo wa kushoto Rafael Correa alie waziri wa fedha wa zamani,anapambana na mhafidhina Alvaro Noboa ambae ni tajiri mkubwa kabisa nchini Ecuador.Katika duru ya kwanza ya uchaguzi hapo Oktoba 15,Noboa alishinda asilimia 26.8 ya kura zilizopigwa kulinganishwa na 22.8 za Correa.Uchunguzi wa maoni uliofanywa mara ya mwisho,umeonyesha kuwa wapinzani hao wawili wanakwenda bega kwa bega.Correa mwenye umri wa miaka 43 ni rafiki wa rais wa Venezuela Hugo Chavez anaefuata siasa za mrengo wa kushoto. Correa,kama Chavez ni mpinzani wa siasa za Marekani.Tajiri Noboa alie na miaka 56 ameahidi nafasi mpya za ajira na nyumba zaidi kwa ajili ya watu walio masikini ikiwa atachaguliwa.